Wimbi la joto kali Ujerumani lachukua maisha ya maelfu kwa wiki mojaMaisha elfu tisa mia sita yalipotea Ujerumani kati ya Juni ishirini na mbili hadi ishirini na nane.

Jumla ya vifo Ujerumani mwaka huu kutokana na joto imefikia elfu kumi na moja mia tisa.

Joto Ujerumani lilipanda hadi nyuzi arobaini, wastani wake ukiwa nyuzi ishirini na sita nukta nne. Wazee wenye umri zaidi ya miaka themanini na tano na wagonjwa sugu ndio waliathirika zaidi.

Vyama vya madaktari na taasisi za afya vimetaka serikali kuanzisha sera za kudumu za tabianchi. Mpango wa kitaifa wa kujikinga na joto unahitajika sana, miji iwe ya kijani, afya ziimarishwe.