Operesheni kubwa ya polisi Bulgaria yasambaratisha kundi hatari la uhalifuWapelelezi walifichua kundi hatari Bulgaria lililohusika na uhalifu wa mazingira na utakatishaji wa pesa.

Kiongozi pamoja na watu wengine wanne walishikiliwa kwa uchunguzi wa kina wa masaa ishirini na manne.

Mmoja anatuhumiwa kutakatisha fedha, euro milioni moja, laki tano, elfu arobaini na nane na hamsini na mbili. Msako mkali ulifanyika nyumba kumi tofauti, chupa zaidi ya elfu moja na mia tano zilikamatwa.

Vilevile, magari ya kifahari, euro elfu sabini taslimu, na vito mbalimbali vilikamatwa wakati wa msako. Gesi hatari kutoka Uchina ziliingizwa kinyume cha sheria, zikasambazwa katika nchi mbalimbali Ulaya.