Ukame na joto kali vyapunguza mavuno ya kilimo nchini Ujerumani mwaka huuJoto kali pamoja na ukame uliokithiri vimesababisha upungufu mkubwa wa mavuno ya nafaka nchini Ujerumani mwaka huu.
Umoja wa wakulima unakadiria kupata tani milioni arobaini na moja nukta tisa za mazao katika msimu huu.
Uzalishaji wa ngano na mazao mengine ya mafuta umeshuka sana kutokana na mimea kukauka mapema mno shambani. Viongozi wa kilimo wameiomba serikali kuu kutoa msaada wa haraka wa kifedha ili kuwasaidia wakulima walioathirika pakubwa.
Mavuno ya matunda kama tufaha yanatarajiwa kupungua sana baada ya joto kali kuchoma mazao hayo mtini mapema. Wataalamu wanasema matunda mengi yameanguka kabla ya kukomaa huku mengine yakiharibiwa vibaya na mvua kubwa za mawe.
