Uholanzi yakazana, yajiandaa na sheria kali kwa watoto wanaotikisa mitandao! Serikali ya Uholanzi sasa inajiandaa kutunga sheria mpya kwa watoto wadogo wanaotengeneza maudhui ya kibiashara mitandaoni.

Mpango huo unapendekeza, watoto wenye umri chini ya miaka kumi na sita watakaozalisha mapato watachukuliwa kama wafanyakazi.

Waziri Aartsen alisema watoto wanageuzwa vyanzo vya kipato, jambo linalotia wasiwasi mkubwa sana. Watoto mitandaoni wataingia chini ya sheria za kazi za watoto, watakaoenda kinyume watapigwa faini.

Sheria itazingatia sana watoto wanaotumika muda mrefu kutengeneza maudhui kwa ajili ya kipato cha pesa. Wizara itaongeza elimu kwa wazazi na kulinda watoto dhidi ya hatari za kisaikolojia na kijamii.